Rabu, 07 Juni 2023

Kiongozi Wa Mbio Za Mwenge Ahimiza Utunzaji Wa Mazingira Zanzibar

Wananchi mbali mbali wa Kaskazini Unguja wakifanya usafi wa mazingira katika hospitali ya kivunge mkoa wa kaskazini Unguja kuelekea maadhimisho ya  siku ya mazingira Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo mei 5. hafla iliyofanyika juni 04,2023.Picha na Fauzia Mussa - Maelezo Zanzibar.

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar. 4/6/2023

Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A wametakiwa kutunza mazingira ili kuhifadhi uoto wa asili nchini.
Akifunga mafunzo ya Mabadiliko ya tabianchi  Skuli ya Mkwajuni Kiongozi wa mbio za mwenge Abdala Shaibu Kaimu amesema utunzaji wa mazingira ni kitu muhimu katika nchi kwani jikalau mazingira hakuna maendeleo.
Amesema hivi sasa mazingira ni mabaya kutokana na wananchi kufanya uharibifu na kuchafua mazingira kutokana na shughuli mbalimbali za  kijamii.
Amefahamisha kuwa mabadiliko ya tabianchi yanarejesha nyuma harakati za kimaendeleo kutokana na shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji na kilimo usiozingatia utunzaji wa mazingira, ukataji wa miti na kutupa taka ovyo.
 Amefafanua kuwa mafunzo yalitolewa yatasaidia wananchi katika kutambua  juu ya uhifadhi wa mazingira na kuepuka uchafuzi unaopelekea kuharibu  mazingira yaliyopo.
 Aidha amewapongeza vijana kwa kukubali kupatiwa elimu na kuwataka kuyafanyia kazi mafunzo hayo.
Akitoa taarifa ya mafunzo Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa Mazingira Wilayani humo Haji Ussi Haji  amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni  kujifunza maana na athari za mabadiliko hayo ili wananchi wafahamu athari hizo.
Wakati huo huo Kiongozi mbio za Mwenge ametembelea Shehia ya Kibeni na kuangalia mradi wa upandaji wa miti na kusifu juhudi za wananchi katika kupambana na uhifadhi wa mazingira .
Amesema yeye binafsi ameridhia mradi huo kwani utawawezesha wananchi wa hapo kujiendesha kiuchumi.
Akitoa taarifa mradi huo mmoja wa wanakikundi cha upandaji wa miti amesema kuwa jumla ya miti 4953 imeatikwa kwa lengo la kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji visipotee.
Hata hivyo wanakikundi cha mradi huo wameshukuru ujio wa Mwenge wa Uhuru kwa kuridhia mradi wao na kuiomba Serikali kuendelea kukiimarisha kikundi hicho ili kurejesha uoto wa asili nchini
Jumla ya miradi minane imekaguliwa na mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo sehemu mbalimbali zimepitiwa na mbio hizo ikiwemo Hospitali ya Kivunge ,  kituo cha Afya Kidagoni na Mradi wa Visima vya maji pale

Smz Inajivunia Ushirikiano Mzuri Ulipo Baina Yake Na India

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na mgeni wake Balozi Mdogo wa India anayefanyia kazi Zanzibar Dr.Kumar Praveen ,aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na mgeni wake Balozi Mdogo wa India anayefanyia kazi Zanzibar Dr.Kumar Praveen ,aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao.
 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya Maji safi na salama ni muhumu katika ustawi wa jamii na maendeleo ya ukuaji wa uchimi Zainzibar.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi mdogo wa India aliepo Zanzibar, Dk. Kumar Praveen, aliefika kujitambulisha.

Rais Dk. Mwinyi alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inajivunia ushirikiano mzuri ulipo baia yake na India na kwamba Zanzibar imekua ikinufaika na fursa mbalimbali kutoka India ikiwemo fursa za masomo ya muda mrefu na mfupi pamoja miradi ya maji.

Pia Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya India kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa SMZ hususan, ufadhili wa Miradi ya maji inayotekelezwa kupitia mkopo wa Benki ya Exim ya India.

Akizungumzia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha IIT, kinachotarajiwa kujengwa Zanzibar kwa Ushirikiano wa Serikali ya India, Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi Praveen kwamba mazungumzo baina ya SMZ na wahadhir kutoka taasisi ya Teknolojia ya “India Institute of Technology (IIT) yanaendelea vizuri na wapo kwenye hatua nzuri ya mpango huo kwaajili ya utekelezaji wake.

Alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeridhishwa na kasi ya uanzishwaji wa taasisi hiyo kwa Zanzibar ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu kwa ushiriano wa pande mbili hizo na wadau wengine wa Serikali na kueleza kuwa wanaunga mkono hatua hiyo itakayoleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya elimu, Zanzibar yatakayonufaisha pia ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Kumar Praveen, Balozi mdogo aliepo Zanzibar aligusia Miradi ya Maji Zanzibar inayofadhiliwa na Serikali ya India, mradi wa Chuo cha Ufundi wa Amali, Pemba pamoja na ufadhili wa masomo kwa watumishi wa Zanzibar nchini India.

Vile vile, Balozi Praveen alimweleza Rais Dk. Mwinyi kuhusu ujio wa Waziri wa Mambo ya nje ya India, Dk. Subrahmanyam Jaishankar anayetarajiwa kuwasili nchini mwezi Julai mwaka huu, kwa ajili ya uzinduzi wa Miradi ya Maji Zanzibar, katika ujio wake huo Dk. Subrahmanyam pia anatarajiwa kufika Dar es Salaam na Dodoma.

Uhusiano wa diplomasia uliopo baina ya Tanzania na India ni wa historia ambapo India ilifungua Ubalozi wake Dar es Salaam mwezi Novemba mwaka 1962 na mwaka 1974 ikafungua ubalozi mdogo Zanzibar.

Ushirikiano baina India na Tanzania umeendelea kuimarika kwa fursa nyingi za maendeleo kupatikana kwa watu wa mataifa mawili hayo.

Tanzania inaongoza kwa kupata msaada wa nafasi nyingi za udhamini wa masomo nchini India kuliko nchi nyenyine yoyote barani Afrika kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya mataifa mawili hayo.

IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR


Wizara Ya Utamaduni,Sanaa Na Michezo Wametukumbudha Mbali Sana :Mhe. Zungu

 
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu amewapongeza Uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuweka bidhaa ambazo ndizo wanazifanyia kazi na kusema imewakumbusha mbali sana.

Naibu Spika Mhe. Zungu amesema hayo Juni 05, 2023 jijini Dodoma wakati akifungua maonesho ya Wizara hiyo na taasisi zake kabla ya kusomwa Bajeti ya mwaka 2023/2024 Bungeni jijini humo.

“Kwa kweli wametukumbusha mbali sana na vitu ambavyo nimeviona, wabunge wengi ambao nao wameviona, kerikil wengi tulikuwa tumeshavisahau, lakini kutokana na kuviona leo ni muhimu wote tukawa na utaratibu wa kivipitia vitu mbalimbali vya utamaduni wa taifa letu,

Tumeona namna nchi yetu ilivyopata uhuru, wapiganiaji wa huuru, rekodi na kumbukumbu zilizowekwa za wapigania uhuru wote wa taifa letu, tumeona speech ya Mwl. Nyerere ya mwaka 1962 Bungeni, ambayo sidhani kama kuna watanzania wengi wameisoma” amesema Naibu Spika Mhe. Zungu.

Ameongeza kuwa Mwl. Nyerere alitumia maneno mazuri ambayo alibainisha kuwa “Ingawa nasema niliapa, kiukweli tuliapa wote”, kila mwananchi amekula kiapo kulingana na maneno ya Mwl. Nyerere.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema wataendelea kushirikiana na Bunge katika masuala yote ya kuboresha kazi za sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuwaletea maendeleo watanzania.

Kama ishara ya ushirikiano mzuri kati ya wizara na Bange, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara hiyo itawapatia wabunge vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na Kamusi Kuu ta Kiswahili toleo la 3 ikiwa ni vitendedea kazi kwa Wabunge wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Katika ufunguzi huo Naibu Spika aliambatana na Waziri mwenye dhamana Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu Saidi Yakubu, wakurugenzi, wakuu wa taasisi pamoja na watumishi wa Wizara hiyo.





Watendaji Wa Serikali Zingatieni Sheria - Mhe.Majaliwa *Asema Lengo Ni Kuiepusha Serikali Kuingia Katika Migogoro

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma

Wazirti Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa idara na taasisi zote za Serikali watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia sheria hususan katika huduma wanazozitoa na miradi wanayoisimamia ili kuiepusha Serikali kuingia katika migogoro ambayo inaweza kuepukika.

“Watendaji wote wa Serikali zingatieni sheria, taratibu na kanuni tulizojiwekea kwenye utekelezaji wa majukumu yetu ikiwemo usimamizi wa mikataba na makubaliano mbalimbali tunayoingia ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima inayoweza kutokea ndani ya Serikali na kusababisha kufunguliwa kwa mashauri ya madai na usuluhishi.“

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Juni 5, 2023) katika Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Uzinduzi wa Mafunzo kwa Mawakili wa Serikali katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. Amewasisitiza Mawakili hao wawe wabunifu katika kuishauri Serikali ipasavyo kuhusu mashauri yaliyopo.

Waziri Mkuu amesema Mawakili wa Serikali wamepewa dhamana kubwa ya kuitetea Serikali katika uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi, hivyo waongeze bidii na juhudi katika utendaji kazi na wafanye kazi kwa uzalendo, weledi na uadilifu.

Serikali kwa upande wake itaendelea kuitengea bajeti ya kutosha Ofisi hii kwa kadri rasilimali zitakavyoruhusu. Vilevile, itaendelea kuipatia rasilimali kerikil ya kutosha sambamba na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwenye maeneo ya kimkakati kama vile mafuta na gesi, uwekezaji, sheria za anga na madini.“

Waziri Mkuu amesema ili kuhakikisha kuwa Serikali inaendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuendelea kujenga mazingira shindani ya kuvutia wawekezaji, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Wizara, Idara na taasisi za Serikali itatue migogoro kwa njia ya majadiliano na maridhiano.

Mheshimiwa Majaliwa amesema faida ya kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano ni pamoja na kupunguza gharama, kuokoa muda na kulinda mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia. “Nisisitize kuwa, bado Serikali yetu inahitaji wawakezaji katika kuchangia ukuaji wa haraka wa uchumi na pato la Taifa.“

Wizara, Idara na Taasisi za Serikali fanyeni kazi kwa karibu Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi yanayohusu Serikali kwani ndiyo yenye mamlaka ya kisheria ya kusimamia mashauri yanayohusu Serikali na Taasisi zake ndani na nje ya nchi.“

Pia, Waziri Mkuu ametoa msisitizo kwa taasisi zote za umma zenye Mawakili wa Serikali kuzingatia suala la utatuzi wa kero za wananchi ili kupunguza mlundikano wa mashauri ambayo hayana ulazima wa kufikishwa Mahakamani hususan katika kipindi hiki cha miaka mitatu ambacho Wizara ya Katiba na Sheria inatekeleza Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria nchini kote “Mama Samia Legal Aid Campaign”

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo ambayo inafanya kazi kwa weledi imeweza kuisaidia Serikali kuokoa zaidi ya shilingi trilioni saba kutokana na kutatua baadhi ya mogogoro kwa njia ya usuluhishi.

Naye, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende amesema baada ya uzinduzi huo wanatarajia kuendesha mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali zaidi ya 600 ili kuwaongezea ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua  Jarida Maalum la Miaka  Mitano ya Ofisi ya Wakili wa Serikali kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 5, 2023. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt  Boniface Luhende na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha  Jarida Maalum la Miaka  Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kulizindua  kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 5, 2023. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt  boniface Luhende na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro ya kutambua mchango wake katika kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kuzungumza katika Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 5, 2023. Katikati ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniface Luhende.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Awaandalia Hafla Ya Kuwapongeza Wachezaji Wa Timu Ya Yanga, Ikulu Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Medali kama ishara ya shukrani kutoka kwa Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said wakati wa hafla ya kuipongeza timu ya Yanga iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji na Makocha wa timu ya Yanga wakati wa hafla ya kuwapongeza kwa kufanikiwa kufika na kucheza mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Shirikisho Afrika (CAF) nchini Algeria. Hafla hiyo ya kuwapongeza Yanga imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi, wachezaji wa timu ya Yanga pamoja na wadau mbalimbali wa michezo wakati wa hafla aliyowaandalia kuwapongeza Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji na Makocha wa Timu ya Yanga wakiwa kwenye hafla ya kupongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam 


Viongozi, wachezaji wa zamani, waandishi wa Habari, batu maarufu, wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa michezo wakiwa kwenye hafla ya kuipongeza timu ya Yanga iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam







Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Mpango Akiwasili Mkoani Tabora Kwa Ufunguzi Wa Umisseta

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Tabora leo tarehe 06 Juni 2023. Makamu wa Rais amewasili Mkoani Tabora kwaajili ya Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanayofanyika katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.


Milango Kwa Wawekezaji Wa Biashara Ya Kaboni

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesema Serikali inaendelea kufungua milango kwa wawekezaji wa Biashara ili kuhifadhi mazingira.

Amesema hayo leo Juni 06, 2023 wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora Dkt. Rashid Chuachua pamoja na ujumbe wake waliomtembelea kwa Kuwasilisha taarifa ya kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwa ajili ya biashara ya kaboni.

Ameupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kuhifadhi misitu na nia yao ya kuwekeza katika biashara ya Kaboni akisema kuwa mbali ya kuhifadhi mazingira lakini pia itawa chanzo cha mapato ya halmashauri.

“Kutokana na Mikataba ya Kimataifa ya Mabadilkiko ya Tabianchi, segi kama nchi tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanafaidika na biashara hii na ndio maana tumeandaa kanuni na mwongozo,” amesema.

Pia, amesema Ofisi ya Makamu wa Rais ipo tayari kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kuwapa uelewa wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini zikiwemo halmashauri kuhusu faida za kupanda miti na kuhifadhi misitu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Chuachua amesema kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwsa ajili ya hewa ya ukaa ni kupata fursa ya biashara hiyo ambayo faida yake itasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wake.

Amesema wilaya ina fursa kubwa ya kuwekeza katika biashara hiyo kwa kuzingato kuwa kilomita za mraba 12,084.5 sawa na asilimia 86 ya eneo lote la wilaya hiyo.

Hivyo amesema kuwa mradi huo ni muhimu kwan utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya halmashauri ambayo kwa asilimi 80 yaekuwa yakitona na mazao ya kilimo.

Dkt. Chuachua ameongeza kwa kusema kuwa mradi utasaidia katika kutunza mazingira ya ardhi oevu ambayo ndio chanzo cha maji katika Mto Malagarasi na Ziwa Tanganyika.  

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amesema kuwa Biashara ya Kimataifa inasimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo kuwezesha nchi wanachama kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Komba amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yanasababisha ongezeko la joto duniani na vipndi vya baridi na mvua kupungua hali inayochangia ukame.

Hivyo amesema misitu ikiwa mingi itasaidia katika kunyonya gesijoto inayochangiwa na shughuli za kibinadamu zikiwemo moshi unaotokana na magari na viwanda.